SHARE

JESSCA NANGAWE

KATIKA kuonyesha kuendelea kutoa shavu kwa wachezaji wake, mwekezaji wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’, ameungana na mashabiki mbalimbali wa Simba kununua fulana zinazouzwa na beki wa timu hiyo, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’.

Tshabalala ameendelea kutumia fursa ya jina lake kuuza jezi maeneo mbalimbali hapa nchini zikiwa na nembo ya jina lake la M15.

Beki huyo amekiri kuwa uuzaji wa nguo hizo umeendelea kuongezeka na kuzidi kumpa matumaini makubwa ya kubuni kitu kingine kitakachomsaidia kuongeza kipato.

Tshabalala alisema anafurahishwa kuona wadau mbalimbali wakimsapoti akiwemo bosi wake Mo hali inayozidi kumpa faraja kila kukicha.

“Ni ktu cha kujivunia sana, mwanzo nilikuwa nachukulia kawaida lakini kadri siku zinavyokwenda nimekuwa nikiona muitikio ukizidi kwa wadau wengi sana, hii inanipa faraja ya kuzidi kuumiza kichwa juu ya kipi nifanye kuongeza kipato,” alisema Tshabalala.

Mbali na Tshabalala wa Simba, straika wa Yanga, Ditram Nchimbi, naye amekuwa akitumia jina lake kuuza fulana zenye nembo yake ya Duma 29.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here