Home Habari ‘MO’ IBRAHIM V YANGA KESHO

‘MO’ IBRAHIM V YANGA KESHO

6204
0
SHARE

NA SAADA SALIM

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Mohammed Ibrahim ‘MO’, kesho anatarajiwa kukutana na Meneja wake, Jamal Kisongo, kwa ajili ya kuangalia mkataba mpya uliowekwa mezani na klabu yake hiyo, na kama hawataridhika nao huenda akatimkia Yanga.

Mkataba wa MO upo ukiongoni na tayari kuna baadhi ya timu zimeonyesha nia ya kumsajili, ikiwamo Yanga, huku Simba nao wakitaka kumwongezea mwingine, licha ya kwamba hatumiki mara kwa mara.

Akizungumza na DIMBA jijini jana, Meneja huyo alisema hatima ya MO kuongeza mkataba Simba itajulikana wiki ijayo, baada ya kukutana na mteja wake huyo.

Alisema alikutana na viongozi wa Simba wakati timu ilipokuwa Mbeya na kuzungumza kuhusu suala la mkataba wa mchezaji huyo na sasa wiki inayoanza kesho anatarajia kukutana na mteja wake ili waangalie kama kuna uwezekano wa kukubaliana na hicho kinachotoka Simba.

“Wakati tunasaini mkataba mara ya kwanza ‘MO’ alinipa baraka zote za kumsimamia kutokana na umri wake, lakini sasa nahitaji kukaa naye kuangalia baadhi ya mambo anayohitaji katika mkataba mpya ambao Simba wamemwandalia.

“Nimsikilize anahitaji nini afanyiwe, pia kuboresha mkataba huo, baada ya hapo nitakutana na viongozi ili kuwapa kile anachohitaji mchezaji kama wataridhika na mahitaji yake, nina imani ataongeza mkataba ikishindikana, Simba itakuwa imefungua milango kwa timu nyingine kuja kunasa saini yake,” alisema Kisongo.

Meneja huyo alisema tayari kuna baadhi ya timu kutoka Morocco, Algeria, Afrika Kusini, Tunisia, Sweden na Serbia zimevutiwa na aina ya uchezaji wa kiungo huyo ambapo haitashangaza akipata dili moja ya nchi hizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here