SHARE

LONDON, England 

KOCHA mkuu wa Tottenham, Jose Mourinho, amesema haitakuwa ngumu kwake kuifundisha timu ya taifa ya Ureno siku moja lakini haipo katika mpango wake wa muda mfupi.

“Niliondoka Ureno mwaka 2004 na bado sijarudi,” aliliambia Fox Sports Brasil. “Kuna watu wanaimani ipo siku moja nitarudi na kuifundisha timu ya taifa na siwezi kujibu ndiyo au la. Nina miaka 57, ni kocha kijana.

Ninajua namna ya kuwanyamazisha wale wanaosema nimechoka kwa sababu nimekuwa kwa miaka mingi nikifundisha katika kiwango cha juu.

“Lakini hapana. Bado sijachoka kufundisha, nimechoka kuwa nyumbani kwa sababu ya covid-19. Mungu akipenda, nina miaka mingi mbele yangu na huwezi jua nini kitatokea. Ni vigumu kusema ndiyo lakini haiwezekani kusema hapana.” 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here