SHARE

NA JESSCA NANGAWE
MWANAMUZIKI Aslay Isihaka ameamua kumtumia mwanaye wa kike Moza katika ngoma yake mpya ‘Moyo Kiburi’ na kudai hatua hiyo imetokana na kuanza kuona kipaji chake.
Akizungumza na DIMBA,Aslay alisema, kitendo cha kumshirikisha binti yake huyo ni kuzidi kumpa hali ya kujiamini kwa kila jambo analotaka kulifanya hata ikitokea akapenda kuja kuwa kama baba yake.
“Kipaji ni mipango ya Mungu, ikitokea Moza amekua msanii kwangu haitanisumbua kwa kuwa yote ni mipango ya Mungu, nimemshirikisha kwenye wimbo wangu kwa kuangalia mambo mengi lakini kubwa ni kumpa moyo wa uthubutu katika kila analotaka kulifanya hata kwenye masomo yake”alisema Aslay.
Staa huyo amesema huenda huo ukawa wimbo wake wa mwisho kwa mwaka huu huku akianza kupanga mikakati mipya ya kuanza mwaka mwingine kwa staili ya aina yake.
Mbali na mtoto huyo, pia wapo watoto wengine wawili wanaoonekana katika ngoma hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here