Home Hadithi MRITHI WA MALINZI HUYU HAPA

MRITHI WA MALINZI HUYU HAPA

0
SHARE

NA MARTIN MAZUGWA

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), jana limekaa kikao cha dharura na kuwakabidhi rasmi Wallace Karia pamoja na  Salum Madadi madaraka ya kulisimamia shirikisho hilo hadi pale wenye nafasi zao watakapomaliza kesi zao.

Karia ambaye ni Makamu wa Rais, atakaimu nafasi ya raisi wakati Madadi ambaye ni Mkurugenzi wa Ufundi atakaimu nafasi ya Katibu Mkuu ili kuziba mapengo ya viongozi hao.

Hatua hiyo inatokana na Rais wa TFF Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake, Selestine Mwesigwa kupelekwa mahabusu wakishutumiwa kwa utakatishaji wa fedha.

Akizungumza na waandishi wa habari jana makao makuu ya shirikisho hilo, Madadi alisema maazimio hayo yamefanyika jana katika kikao cha dharura na wamefanya hivyo kwa mujibu wa katiba ya TFF,  kifungu cha 35(1) pamoja na 36 ambacho ndicho kilichotumika kuwakabidhi nyadhifa hizo.

“Nafasi hizi zitadumu hadi pale kesi itakapokwisha kabisa na viongozi hao watakapokuwa huru ndipo wataendelea na shughuli zao kama kawaida.

“Maazimio haya yamefanyika kuokoa utendaji kazi wa shirikisho kwani kuna mambo mengi yamesimama mara baada ya tukio hili, ikiwamo suala la uchaguzi mkuu pamoja na kikosi cha timu ya taifa kilichopo katika mashindano ya COSAFA,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here