Home Habari MRITHI WA MASOUD DJUMA SIMBA HUYU

MRITHI WA MASOUD DJUMA SIMBA HUYU

3856
0
SHARE

CLARA ALPHONCE NA SAADA SALIM


KAULI ya kaimu Rais wa Klabu ya Simba, Salim Abdallah, maarufu kama Try Again, kwamba suala la Masoud Djuma, kubakia kwenye Klabu hiyo halina afya, ni dhahiri Mrundi huyo ameshafungashiwa kila kilicho chake na sasa anayekuja kurithi mikoba yake ameshajulikana.

Akizungumza jana asubuhi na kituo cha Azam TV, Try Again alikiri kwamba kuna hali ya sintofahamu kati ya Djuma na Kocha Mkuu Patrick Aussems, na kwamba watatangaza maamuzi magumu muda wowote.

Alisema, Djuma amekuwa hana mawasiliano mazuri na Aussems, jambo ambalo limepelekea kuleta msuguano usiokuwa na tija, pia akikumbushia namna kama hiyo alipokuwa na kocha mwingine, Pierre Lechantre.
“Ni kweli kumekuwa na matatizo ambayo yamekuwa yakijirudia baina ya Masoud Djuma na benchi la ufundi, haswa kwa makocha wakuu, akiwamo Joseph Omog na Pierre Lechantre aliyeondoka.

‚ÄúTumekuwa tukifanya jitihada za kutatua tatizo hilo bila mafanikio, siwezi kueleza mengi kwa sasa, ila tutakuja na tamko rasmi baadaye, tunachoweza kusema ni kuwa suala la Djuma kubaki Simba halina afya nzuri”, alisema.

Bosi huyo wa Simba ameeleza kuwa …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la DIMBA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here