Home Burudani MSAMI ATOA MASHARTI YA KUFANYA KOLABO

MSAMI ATOA MASHARTI YA KUFANYA KOLABO

1004
0
SHARE
NA JESSCA NANGAWE

MSANII wa muziki Bongo, Giovanni Msami maarufu kama Msami Baby, amedai kuwa kwa sasa hayupo tayari kufanya kolabo na msanii yeyote labda aahidiwe dau kubwa lenye faida kwake.

Mwimbaji huyo anayefanya vizuri kwa sasa kwenye gemu, amesema amechukua uamuzi huo ili kufanya zaidi kazi zake binafsi bila kuingiliwa na mtu.

“Kwanza niseme tu sipo tayari kuonekana kwenye video ya msanii yeyote, iwe kwa staili yoyote au kucheza, kuonekana tu nimeuza sura, yaani siwezi kuonekana labda kuwe na faida kubwa sana ninaipata,” alisema Msami.

Ameongeza kuwa kwa sasa yupo makini kufanya muziki wake na kazi ya uchezaji amewaachia watu wengine kwa sababu ameona umefika wakati wa kufanya hivyo ili na wengine wapate nafasi hiyo pia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here