Home Habari MSUVA AMTETEA LWANDAMINA

MSUVA AMTETEA LWANDAMINA

443
0
SHARE

Na CLARA ALPHONCE,

WINGA machachari wa Yanga, Simon Msuva, amewasikia mashabiki wa Yanga wakipinga kelele kutokana na uwezo wa Kocha George Lwandamina na kuwaambia wampe muda, kwani anaweza kuvunja rekodi ya Kocha Hans Pluijm, aliyoiweka katika klabu hiyo.

Msuva aliwachambua makocha hao na kusema wote ni makocha bora na kila mmoja ana falsafa yake ya ufundishaji, ila kwa upande wake hajaona tofauti kubwa iliyopo.

“Mimi naona sawa, kwani alipokuwapo Pluijm alikuwa ananichezesha namba na hata Lwandamina ananichezesha namba hiyo hiyo, tofauti iliyopo ni mfumo tu.

“Ila kinachotakiwa ni kumpa muda kocha Lwandamina, kwani anaweza kuifikisha mbali Yanga na kufikia rekodi ya Pluijm au kumpita, ila kama sisi wachezaji tutakubali kujituma na kufanya kazi.”

Hivi karibuni kulikuwa na kauli mbalimbali za wanachama na wapenzi wa Yanga kuhusu uwezo wa Lwandamina, baada ya timu hiyo kutokufanya vizuri katika michezo yake kadhaa ya Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ubingwa

Hata hivyo, mshambuliaji huyo aliongeza kuwa, kuhusu Yanga kuchukua ubingwa msimu huu, lipo wazi, japo hapo nyuma walikumbwa na changamoto ya majeruhi, lakini wanashukuru Mungu kila siku zinapozidi kwenda wajeruhi wamekuwa wakiimarika.

Michezo ya kimataifa

Msuva alisema kilichofanya watolewe kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na timu ya Zanaco ya Zambia, ni kutotumia vizuri uwanja wa nyumbani, baada ya kupata sare ya mabao 1-1.

Alisema sasa wanakwenda kukutana na MC Alger ya Algeria ambapo msimu huu wanataka kumaliza unyonge, kwani wamekuwa wakipoteza mechi wanapokutana na timu za Kaskazini mwa Afrika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here