Home Habari MSUVA, BANDA WAPISHANA

MSUVA, BANDA WAPISHANA

708
0
SHARE
NA JESSCA NANGAWE

WAKATI beki wa Baroka FC ya Afrika Kusini, Abdi Banda, ameondoka nchini juzi kurejea kwenye klabu yake, amejikuta akipishana na Simon Msuva ambaye anarejea Tanzania kwa ajili ya mapumziko mafupi.

Banda alikuwa nchini kwa mapumziko ya wiki moja kwa ajili ya kupisha Sikukuu za Krismasi, amerejea juzi Afrika Kusini ili kujiandaa na Ligi Kuu nchini humo.

Kwa upande wa winga Msuva ambaye anaichezea klabu ya Al Jadida ya nchini Morocco, anatarajia kurudi nchini kesho baada ya ligi yao kusimama kwa muda.

Msuva amesema kwamba ligi ya Morocco inakwenda mapumzikoni naye anarejea nyumbani kwa mapumziko na kujipanga kwa mzunguko wa pili.

“Natarajia kurudi nyumbani kuanzia Alhamisi kwa mapumziko baada ya mzunguko wa kwanza Ligi Kuu huku na pia kujipanga kwa mzunguko wa pili kabla ya kurudi kambini,” alisema.

Msuva anaweza kuwa kwenye mapumziko marefu, kwa sababu michuano yote nchini Morocco sasa itasimama kupisha Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), zinazohusisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani pekee, zinazotarajiwa kuanza Januari 13 hadi Februari 4, mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here