Home Burudani MUME WA ZARI AZIKWA DIAMOND MTINI!

MUME WA ZARI AZIKWA DIAMOND MTINI!

314
0
SHARE

NA MWANDISHI WETU,

MWANAMUZIKI wa kizazi kipya Naseeb Abdul, maarufu kama Diamond amezua maswali kibao kwa mashabiki kutokana na kuwepo taarifa ya kuhudhuria mazishi ya mume mwenzake Ivan Ssesemwanga aliyezikwa jana lakini baadaye asionekane.

Maswali zaidi yalihusu taarifa za kwamba Diamond angehuhuduria mazishi hayo yaliyofanyika katika kitongoji cha Kayunga, Uganda lakini hadi shughuli zote zinakamilika msanii huyo maarufu hakuonekana.

Katika hali iliyotia simanzi ni pale mke wa Diamond Zari Hassan alipoonekana mpweke, huku mashabiki wakiulizana juu ya tikio hilo.

Dimba lilimtafuta mmoja wa viongozi wa kampuni ya Wasafi, Babu Tale lakini hakupatikana.

Baadhi ya mashabiki wa msanii huyo waliozungumza na Dimba Jumatano, jijini Dar es salaam, walilalamikia kitendo cha mkali huyo kufanya shoo wakati kuna msiba unaomuhusu.

Hata hivyo habari za ndani zilizolifikia Dimba muda mfupi likiekekea mitamboni zinasema, Diamond alishindwa kuingia Uganda baada ya kuzuiliwa muda mfupi baada ya kumaliza onyesho lake kubwa jijini Nairobi, haikuelezwa sababu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here