SHARE

NA WINFRIDA MTOI
KOCHA Mkuu wa Mbeya City Juma Mwambusi amejiuzulu kukinoa kikosi hicho kutokana na mwenendo mbaya katika Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mwambusi alirejeshwa Mbeya City msimu huu baada ya kuachana na Azam alikokuwa kocha msaidizi, lakini tangu arudi kuinoa timu hiyo ameshindwa kuipa matokeo bora kwani katika mechi 12 alizocheza ameshinda moja tu.
Taarifa iliyotolewa jana na uongozi wa klabu hiyo, imeeleza kuwa Mwambusi aliwasilisha barua ya kuomba kujiuzulu tangu Novemba 26, mwaka huu ili kulinda maslahi mapana ya timu hiyo.
Kutokana na kujiuzuru kwa Mwambusi, bodi ya timu hiyo imekabidhi majukumu kwa kocha msaidizi, Mohamed Kijuso wakati mchakato wa kumtafuta kocha mwingine ukiendelea.
“Bodi inamshukuru mwalimu Juma Mwambusi kwa mchango wake mkubwa kwa maendeleo ya timu na bado inahitaji ushauri na uzoefu wake katika tasnia ya michezo”, ilisema taarifa hiyo iliyolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Mbeya James Kasusura.
Katika msimamo wa ligi kuu, timu hiyo inashika nafasi ya 19 na pointi saba, baada ya kucheza mechi 12, imeshinda moja, sare tano na kupoteza sita.
@@@@@@@@@

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here