Home Michezo Afrika MZAMBIA KUZIHUKUMU MISRI, CAMEROON

MZAMBIA KUZIHUKUMU MISRI, CAMEROON

415
0
SHARE

LIBREVILLE, Gabon

MWAMUZI raia wa Zambia, Janny Sikazwe, ametangazwa kuwa mwamuzi wa kati katika mchezo wa Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon), mchezo utakaozikutanisha Cameroon na Misri.

Sikazwe (37), mwaka 2015 alitangazwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kuwa ndiye mwamuzi bora wa mwaka.

Mwamuzi huyo mwenye beji ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), alishachezesha mechi ya Klabu Bingwa ya Dunia baina ya Real Madrid na Kashima Antlers, Desemba mwaka jana.

Fainali za mwaka huu za Afcon zinafanyika nchini Gabon huku baadhi ya timu zikiondolewa mapema zilizokuwa zikipewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa msimu huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here