Home Burudani NADAL KUMVAA KHACHANOV NUSU FAINALI ROGERS CUP

NADAL KUMVAA KHACHANOV NUSU FAINALI ROGERS CUP

4858
0
SHARE

TORONTO, Canada


BINGWA mara 16 wa taji la Glandslams, Rafael Nadal, ametinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Rogers Cup na anatarajia kumvaa Karen Khachanov, ili aweze kutinga fainali.

Nadal ametinga hatua hiyo baada ya kupata ushindi wa seti 2-1 na pointi 2-6, 6-4 na 6-4 mbele ya mbishi Marin Cilic ambaye alianza vyema seti ya kwanza.

Wakati Nadal akiendelea kurejea taratibu katika ubora wake, naye kinda, Tsitsipas,19, ametinga hatua hiyo baada ya kumbwaga Dominic Thiem na kuvunja rekodi ya raia huyo wa Hispania ya kushinda mbele ya mkali anayeshika nafasi ya tatu kwa ubora.

Nadal alifanya hivyo mwaka 2006 katika michuano ya Monte Carlo, hivyo kinda huyo amevunja rekodi hiyo iliyodumu kwa miaka 12.

Katika nusu fainali nyingine, Tsitsipas, anatarajia kumvaa mkali anayeshika nafasi ya nne katika viwango vya ubora, Kevin Anderson, ambaye ameingia hatua hiyo baada ya kuibuka na ushindi mbele ya Grigor Dimitrov kwa seti 2-0 za pointi 6-2, 6-2.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here