Home Habari Namungo yamsajili kiboko ya Manula

Namungo yamsajili kiboko ya Manula

414
0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE

UONGOZI wa Namungo FC ya Lindi imemsajili mshambuliaji wa Alliance FC, Bigirmana Blaise, kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Ikumbukwe Bigirimana kabla ya kutua Alliance alikuwa Stand United ambapo kipa wa Simba Aishi Manula anamkumbuka jinsi alivyomtungua wakati wakicheza na Stand United na matokeo kumalizika kwa 3-3 jijini Dar es Salaam.

Ofisa Habari wa Namungo, Kidamba Namlia, alisema moja ya mipango yao ni kupata wachezaji wenye uzoefu ambao wataipa nguvu safu ya ushambuliaji.

“Mpango uliopo kwa sasa ni kuboresha kikosi chetu, tumeanza na Blaise wengine wanafuata kwasababu kazi kubwa tunayoifanya ni kusajili wachezaji wenye uzoefu watakosaidia kuleta ushindani msimu ujao,” alisema.

Namlia aliongeza hawataki wachezaji wa majaribio ama wale ambao uwezo wao ni wa kubahatisha kwasababu Ligi Kuu Bara sio sawa na Ligi Daraja la Kwanza.

Namungo ni miongoni mwa timu zilizopanda daraja msimu huu na sasa inajiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania bara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here