SHARE

NA JESSCA NANGAWE


BAADA ya mume wa Shamsa Ford aitwaye Chid Mapenzo kuelezea hisia zake za kutaka kurudiana na mke wake huyo, rapa Nay wa Mitego amemwangukia mrembo huyo na kutaka amsikilize mumewe.

Ndoa ya wawili hao Shamsa na Chid ilivunjika hivi karibuni na kila mmoja kuendelea na maisha yake kama zamani.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Nay wa Mitego alisema, tayari Shamsa na Chiddi walishaanza safari ya maisha ya ndoa na mkosaji amejutia kosa hivyo ni vyema mrembo huyo akarudisha moyo wa imani na kurejea kwa mume wake.

Wale ni wanandoa, nadhani Chiddi amefanya tendo la busara kuomba msamaha wazi wazi, nimuombe tu Shamsa afikirie hilo na kurejesha moyo wa imani ili warudi na kuendeela kujenga maisha yaoîalisema Nay.

Nay wa Mitego na Shamsa inadaiwa waliwahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi miaka ya nyuma na kisha kutengana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here