SHARE
Ettiane Ndayiragije

NA JESSCA NANGAWE

BAADA ya Tanzania kupangwa kundi D katika michuano ya CHAN 2020, kocha mkuu wa timu hiyo Ettiane Ndayiragije amesema hana hofu na wapinzani wakekwani jmabo muhimu ni wao kufanya maandalizi ya nguvu.

Stars inatarajia kuingia kambini mwezi ujao, tayari kwa maandalizi ya kujiandaa na michuano hiyo ya fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN.

Kikosi cha Stars kimepangwa kundi D na timu za Zambia, Guinea, pamoja na Namibia huku majirani zao Uganda wakipangwa na Rwanda, Togo, na Morocco.

Akizungumza Ndayiragije, alisema, hana hofu na timu anazokwenda kukutana nazo kwa kuwa kikubwa anachotambua yeye ni maandalizi ya timu na jinsi wachezaji watakavyojituma uwanjani.

ìKikubwa ni maandalizi na kumuomba Mungu, tutimize majukumu yetu kadri tunavyoweza, naamini maandalizi ya mapema na jinsi wachezaji watakavyokua wanajituma ndiko kutatuvushaîalisema Ndayiragije.

Bao la straika wa sasa wa Yanga Ditram Nchimbi lilitosha kuisaidia timu hiyo kusonga mbele baada ya kuwaacha Sudan kwa mabao 2-1 kwenye uwanja wa Elmnerreik Omdurman nchini Sudan.

Michuano hiyo inatarajia kufanyika nchini Cameroon mapema mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here