SHARE

LAGOS, Nigeria

SAA chache zimetosha kutikisa kiwanda cha burudani Barani Afrika na hasa nchini Nigeria, baada ya kuibuka kwa ripoti zilizodai kuwa mkali wa muziki, Davido, alikaribia kuachana na mkewe, Chioma.

Ripoti hizo zilieleza kuwa wawili hao walianza kwa kila mmoja kufuta urafiki na mwenzake katika mtandao wa Instagram, huku wakiacha maswali kwa mashabiki wao.

Lakini, katika mahojiano yaliyomhusisha bosi wa lebo ya GoldenBoy Entertainment, King Patrick, alisema kuwa msanii Peruzzi, ambaye alikuwa naye kabla ya kumzunguka na kwenda lebo ya Davido, DMW, alitoka kimapenzi kwa siri na Chioma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here