Home Burudani NEY WA MITEGO AFICHUA SIRI YA TATTOO

NEY WA MITEGO AFICHUA SIRI YA TATTOO

875
0
SHARE

Na GLORY MLAY

MKALI wa muziki wa hip hop nchini, Emmanuel Elibariki ‘Ney wa Mitego’, amesema mwili wake umepambwa na tattoo zaidi ya nane ambazo kila moja ina maana yake.

Ney ameliambia DIMBA kwamba, amejichora tattoo hizo baada ya kuvutiwa na watu mbalimbali waliokuwa wakizichora katika miili yao.

“Nina tattoo zaidi ya nane kwenye mwili wangu, nyingi zipo kwenye mkono wa kushoto na nyingine zipo mgongoni ambazo watu hawawezi kuziona, nilikuwa napenda sana mtu akijichora ndiyo maana nikaamua kuchora,” alisema.

Alisema tattoo zilizopo kwenye mkono wake wa kushoto, ya kwanza ni gitaa, ambayo ina maana ya muziki, kwakuwa anapenda muziki ndiyo maana akaichora, ya pili inaonyesha ala za muziki, huku ya tatu ikionyesha dragoni, ambaye ni nyoka mkubwa ambaye anampenda.

Alifafanua kwamba, tattoo ya nne inaonyesha alama ya nembo ya studio yao ya Free Nation na ya tano iliyopo mkono wa kulia inaonyesha nanga na ndiyo ya kwanza kuichora, huku ya sita ikionyesha nyota, ikimaanisha kwamba yeye ni star katika muziki hapa nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here