Home Michezo Kimataifa NEYMAR, MBAPPE, CAVANI KAZI NDIYO IMEANZA HIVYO

NEYMAR, MBAPPE, CAVANI KAZI NDIYO IMEANZA HIVYO

708
0
SHARE

METZ, Ufaransa

USIKU wa kuamkia jana klabu ya PSG iliutambulisha rasmi utatu wao hatari na wa thamani duniani, unaoongozwa na Neymar (euro mil.222), Kylian Mbappe (euro mil.180), na Edinson Cavani (euro mil.63).

Katika mchezo huo wa Ligue 1 waliocheza dhidi ya Metz, PSG waliibuka na mabao 5-1, huku mastaa hao watatu wote wakicheka na nyavu.

Ni kosa kubwa kusema PSG imekamilika kila idara, kwani bado kiufundi kuna wachezaji ambao wana-miss pale, lakini kwa kiwango cha hali ya juu walichoonesha juzi, ni wazi Waarabu wa Qatar waliona kitu wakati wanazitoa fedha zao na kuwanunua mastaa hao watatu.

Timu hiyo ilianza na kikosi ambacho kiukweli hakikuwa na uwiano sawa, ambapo ilianza na mfumo wa 4-2-2-2, wakiwa na mafowadi wanne.

Kwa timu na namna hiyo, ni ngumu sana kunyakua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, kama una washambuliaji wakali, na mabeki wa kuungaunga, jukumu zito lipo kwa kocha Unai Emery, kutafuta namna ya kuiweka sawa timu yake.

Hata hivyo, kwenye Ligue 1, PSG wana nafasi kubwa ya kuzitesa timu za huko Ufaransa, kwani hakuna mabeki wenye uwezo wa kuzuia balaa la akina Neymar, Mbappe, Cavani na Julian Draxler, ambao hawatakuwa na jukumu lolote la kukaba zaidi ya kushambulia tu.

Bao la kwanza la mtanange huo lilipachikwa wavuni na Cavani, ambapo Neymar aliukamata mpira akiwa mita chache nyuma ya penalti boksi, akawaona Mbappe na Cavani wakivizia eneo la hatari na kuipenyeza pasi iliyonaswa na kupelekwa nyavuni.

Dakika chache baadaye, Metz walisawazisha kutokana na uzembe wa mabeki wa PSG, na kuufanya mchezo uende mapumziko ngoma ikiwa 1-1. Kiukweli, lile ni aina ya bao ambalo PSG kama wasipokuwa makini msimu huu kwenye michuano ya Ulaya, watafungwa sana. Huku kwenye ligi wala hakuna shida.

Kipindi cha pili, Mbappe aliwafurahisha mashabiki wa PSG baada ya kupachika bao la pili, akiuwahi mpira uliozuiliwa na beki wa Metz aliyeiharibu pasi yake kwa Neymar, hapo sasa ndipo balaa lilipoanza.

Usiku wa juzi, Neymar alikuwa akizunguka sana kwenye shimo akijaribu kufungua vyumba kwa wenzake, hasa Mbappe na mabeki wa pembeni. Au, kwa jinsi mchezo ulivyokuwa, Mbappe na Neymar walikuwa wakijituma mno kutengeneza nafasi, ambapo walipokezana nafasi hapa na pale.

Dakika chache baadaye, Neymar akapachika bao la tatu, la nne kwake yeye msimu huu. Kabla ya Cavani kufunga la nne, Lucas Moura akafunga la tano. Na PSG wakautambulisha utatu wao hatari kuwa ndio umeanza kazi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here