Home Makala Ngassa, Mpalile tokeni hadharani muombe radhi

Ngassa, Mpalile tokeni hadharani muombe radhi

4068
0
SHARE

NA MAREGES NYAMAKA

USIKU wa Jumapili wiki iliyopita, straika wa Liverpool, Divock Orig, raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Kenya, aliibuka shujaa wa mchezo wa Ligi Kuu England kati ya timu yake dhidi ya Everton, maarufu kama ‘Merseyside Derby’.

Hatua hiyo inatokana na kufunga bao pekee la ushindi dakika za lala salama akitokea benchi na kuiwezesha timu yake kujiweka kwenye nafasi nzuri katika mbio za ubingwa.

Ndicho alichokifanya Amis Tambwe wa Yanga aliyetokea benchi na kufanikiwa kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Tanzania Prisons mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Sokoine.

Miguu ya Tambwe ilikuwa inaifanya Yanga kuendelea kuvuna pointi tatu ndani na nje katika michezo 13 kati ya 15, huku miwili, wakiwashindwa Ndanda na Simba pekee mechi zilizomalizika kwa sare.

Kabla ya ushindi huo wa Yanga, mabao yote yalifungwa ndani ya dakika 15 za mwisho kipindi cha pili dakika tatu za mwisho, kipindi cha kwanza, hasa dakika tatu za wingu jeusi lilichukua nafasi.

Ilikuwa ni baada ya mwamuzi kuashiria pigo la penati upande wa Tanzania Prisons baada ya beki wa kati wa Yanga, Andrew Vicent ‘Dante’ kumchezea faulo mmoja wa wachezaji wa Prisons katika eneo la hatari.

Utulivu wa wachezaji wa Yanga ulikosekana kabisa kundi kubwa la wachezaji, likimzonga mwamuzi, huku nahodha Juma Abdul aliyetakiwa kuwazuia wachezaji wenzake katika hilo, hakufanya hivyo. Tatizo.

Feisal Salum ambaye bado ni kijana mdogo, yeye ndiyo akageuka kuwatuliza wenzake. Ni nidhamu kubwa sana katika soka kwa alichokifanya tofauti na kilichofanywa na mkongwe katika soka, Mrisho Ngassa.

Kwa nini nimemtaja Ngassa? Dakika chache baadaye baada ya hilo tukio la penalti kupita, alichokifanya ni utovu wa nidhamu tena wa hali ya juu mno kumpiga kichwa mchezaji wa timu pinzani, huku akiwa hana mpira.

Unajiuliza nini kilimkumba Ngassa, alipandwa na mdudu gani kichwani? Unaenda mbali zaidi, kuna neno baya alitolewa na mhusika? Kwa vyovyote vile winga huyo ambaye amekuwa kioo kwa vijana wengi bado hakwepi kosa.

Ni kuigharimu timu bila sababu yenye tija kwa nafasi iliyopo kileleni mwa msimamo. Ni rahisi kumuelewa mapema kwa kosa kama hilo likiwa limefanywa na Maka Edward, Paul Gofrey pamoja na wachezaji kadhaa ambao wanachipukia, lakini si Ngassa.

Mbaya zaidi kilichofanywa na Ngassa ndani ya sekunde chache hizo hicho kinafanywa na nahodha wa Prisons, Lauriani Mpalile. Ajabu nyingine ya wanaonekana vioo kwa vijana wanaochipukia kugeuka kuwa karaha.

Mpalile ambaye kwenye ligi ni zaidi ya msimu wa 10 sasa kumfuata Ngassa na kutaka kulipiza kisasi, ilimpunguzia kabisa sifa zake za kuvaa kitambaa kuwaongoza wenzake. Nidhamu aliiweka pembeni.

Mbali na soka ambalo linahitaji nidhamu, lakini pia bado yeye ni askari Magereza ambapo nidhamu ndiyo silaha kubwa kwa kila hatua. Majibu rahisi ya damu ikichemka vitu hivyo vinatokea. Hapana.

Wawili hao itapendeza zaidi kwa kutumia njia yeyote ile kuomba radhi katika hili na si kujificha katika kichaka cha Zinedine Zidane aliyempiga kichwa Daniela Materazzi 2006 katika mchezo wa Kombe la Dunia, kwani hata yeye aliomba radhi. Muungwana ni vitendo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here