Home Habari NGOMA CHINI YA UANGALIZI MAALUMU

NGOMA CHINI YA UANGALIZI MAALUMU

696
0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE,

STRAIKA wa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, Donald Ngoma, amewekwa chini ya uangalizi wa matibabu maalumu kutokana na majeraha yanayomkabili.

Ngoma aliumia mguu hivi karibuni katika mchezo wa ligi kuu baina ya Yanga na Stand United  na kulazimika kuanza upya matibabu, ambapo kuumia kwake kumewatia hofu mashabiki wa timu hiyo asije akaukosa mchezo dhidi ya Ngaya De Mbe na ule dhidi ya Simba.

Daktari wa Yanga, Edward Bavu, ameliambia DIMBA Jumatano kuwa Ngoma kwa sasa anaendelea vyema na matibabu na mazoezi ya mguu ikiwezekana auwahi mchezo dhidi ya Wacomoro au ule na Simba utakaopigwa Februari 25.

“Ngoma anaendelea na matibabu na yupo chini ya uangalizi maalumu, pia ameanza mazoezi mepesi  peke yake, tunazidi kuangalia hali yake itakuwaje kabla ya kuelekea Comoro,” alisema daktari wa yanga Bavu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here