Home Habari NIDHAMU YAWABAKIZA TAMBWE, KAMUSOKO

NIDHAMU YAWABAKIZA TAMBWE, KAMUSOKO

563
0
SHARE

CLARA ALPHONCE NA HUSSEIN OMAR,

STRAIKA Amis Tambwe na kiungo Thaban Kamusoko, ni nyota pekee wa Yanga wenye uhakika wa kubaki msimu ujao kwenye kikosi cha timu hiyo baada ya mabosi wa timu hiyo kukunwa na uwezo wao uwanjani, ukichagizwa na nidhamu.

Katibu Mtendaji wa Yanga, Charlse Boniface Mkwasa, ameliambia DIMBA kwamba, nyota hao tayari wamepenya kwenye chekeche la wachezaji wa kimataifa ambao klabu hiyo imepanga kuwaboreshea maslahi yao.

Alisema, Tambwe na Kamusoko ni wachezaji walioitumikia Yanga kwa moyo wa uzalendo kipindi cha mpito cha mtikisiko wa kiuchumi waliokuwa nao, kitu ambacho kimewajengea heshima na kuufanya uongozi uone umuhimu wa kuwabakisha kundini.

“Hata katika Biblia imeandikwa asiyefanya kazi na asile, na kila mtu atakula kwa jasho lake, hivyo hata sisi tutaangalia zaidi kujituma na nidhamu ya mchezaji katika kuboresha maslahi kwenye mikataba yao,” alisema.

Alipoulizwa kuhusu nyota ambao mikataba yao inaelekea ukingoni, Mkwasa alisema kuwa jukumu hilo la kujua nani anaondoka na nani anabaki limeachwa kwenye benchi la ufundi, sambamba na kamati ya mashindano.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here