Home Habari NIKI WA PILI AANIKA SIFA ZA MKEWE MTARAJIWA

NIKI WA PILI AANIKA SIFA ZA MKEWE MTARAJIWA

6239
0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE


RAPA wa muziki wa hip hop nchini, Niki wa Pili, amefunguka kuhusu sifa za mke wake mtarajiwa huku akitaja vigezo muhimu anavyovutiwa navyo.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Niki wa Pili alisema sababu kubwa alivyovutiwa nayo kwa mchumba wake wa sasa ni upendo pamoja na kumjua Mungu, vitu ambavyo amekuwa akivipa nafasi kwenye maisha yake.

“Nashukuru nina mwanamke mwelewa, ana upendo na pia anamjua Mungu..kwangu hivyo ni vigezo ninavyovipa nafasi sana,” alisema Niki wa Pili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here