Home Burudani ‘NIMECHOKA’ YA HARMONIZE YADAIWA DONGO KWA WOLPER

‘NIMECHOKA’ YA HARMONIZE YADAIWA DONGO KWA WOLPER

498
0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE
MSANII kutoka kundi la WCB, Rajab, maarufu kama ‘Harmonize’, ameachia ngoma mpya inayoitwa ‘Nimechoka’, huku ndani yake akizungumzia malumbano yanayowahusu wapenzi walioachana.
Harmonize ameliambia DIMBA kuwa, wimbo huo ametoa kwa faida ya wengi na si tu kwa maisha aliyoyapitia yeye, bali ni ujumbe kwa watu wote wanaopitia hali kama hiyo ya mahusiano.
“Wapo wapenzi walioachana, lakini kila kukicha wanazungumzia mapenzi ambayo yamepita, tena kwa ubaya na kutengeneza mazingira ya kukujengea chuki katika jamii, nadhani huu wimbo ni maalumu kwao,” alisema Harmonize.
Aidha, aliongeza kuwa, hayupo katika malumbano na mtu na anafanya kazi kama sehemu ya kutoa elimu kwa mashabiki zake, hivyo asilaumiwe kwa lolote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here