Home Burudani NISHA: NAUMIZA KICHWA KUCHEKESHA WATU

NISHA: NAUMIZA KICHWA KUCHEKESHA WATU

664
0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE,

MSANII wa vichekesho nchini, Salma Jabu, maarufu kama ‘Nisha Bebe’, amesema humchukua muda mwingi kutafakari nini afanye ili kuboresha kazi yake ya uchekeshaji, kwani sanaa hiyo kwa sasa ina ushindani mkubwa.

Nisha, ambaye kwa sasa amejizolea umaarufu mkubwa kupitia sanaa yake ya uchekeshaji, amekiri kuwa yeye ni miongoni mwa wanawake wachache waliojaliwa kuwa na kipaji cha kipekee katika sanaa hiyo.

Akizungumza na DIMBA, msanii huyo alisema tofauti na watu wanavyodhani, yeye amekuwa akitumia muda mwingi na akili sana katika kutafakari nini afanye ili aweze kufikisha ujumbe kwa jamii inayomzunguka.

“Unajua kuna watu wanadhani uchekeshaji ni kazi ndogo, hakuna kazi ngumu kama hii katika uigizaji, unajua kumfanya mtu mpaka acheke si kazi ndogo, ukweli naumiza sana akili kumchekesha mtu, pia ushindani wa sasa kwenye soko ni mkubwa, hivyo ubunifu unapaswa uzingatiwe sana,” alisema Nisha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here