Home Habari Niyonzima afunguka ‘atakachomis’ Bongo

Niyonzima afunguka ‘atakachomis’ Bongo

0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE

PAMOJA na kiungo wa zamani wa Simba, Haruna Niyonzima kurejea nyumbani na kusaini na klabu ya As Kigali, amefunguka na kudai kwamba, Maisha ya soka la Tanzania kwake  yamempa elimu kubwa sana na atakachokumbuka zaidi ni ukarimu wa Watanzania.

Niyonzima mbaye alizichezea Simba na Yanga kwa nyakati tofauti, tayari amesajili na klabu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Akizungumza na DIMBA Niyonzima alisema, anaamini maisha ya soka ni safari ndefu hivyo kwake haoni taabu kucheza sehemu yoyote.

“Nimejifunza mengi sana nikiwa Tanzania lakini kubwa ni ukarimu wao, naamini maisha ya soka ni safari ndefu na ninaamini nitacheza sehemu yoyote, kubwa nimejifunza mambo mengi mazuri nikiwa Tanzania na yatanisaidia katika hatua nyingine ya soka langu,”Alisema Niyonzima.

Aidha alisema kurudi kucheza hapa nchini itategemea na mkataba wake pamoja na mipango ya Mungu kwani yeye kama mchezaji anacheza popote na kikubwa kwake ni kuendeleza kipaji chake.

Aliongeza kuwa, bado ataendelea kuwa na ukaribu na wachezaji wenzake  pamoja na viongozi wake kwa kuwa ni watu waliochangia mafanikio yake ndani na nje ya uwanja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here