SHARE

NA JESSCA NANGAWE

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga Haruna Niyonzima amesema licha ya mpira kuwa biashara kwake, lakini kitendo cha kuitosa timu hiyo mwaka 2017 na kuhamia Simba hatakisahau maishani mwake kwa namna alivyopata wakati mgumu wa maisha.

Niyonzima ambaye alisajiliwa na Yanga mwaka 2012 akitokea klabu ya APR ya Rwanda pia amekiri kuwa mpaka sasa hakuna mchezaji aliyepokewa kwa kishindo kama yeye kutokana na aina ya mapokezi aliyoyapata.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Niyonzima alisema, alichekelea kutua Simba kutokana na mkwanja mnono waliokuwa wamemtengea lakini pesa zile aliziona chungu kutokana na wakati alioupata kutoka kwa mashabiki wa Yanga.

Alisema,mashabiki wa Yanga walikua wakimkejeli na kumtolea maneno machafu kila alipokua anakwenda kitu ambacho kwake kilimpa wakati mgumu wa kufurahi maisha yake ndani ya Simba.

Mpira kwangu ni biashara lakini kile kitendo cha kwenda Simba kiliniweka kwenye wakati mgumu sana, nilipata pesa lakini sikuwa na amani, kila ninapopita kwangu ni matatizo, mashabiki wa Yanga hawakuniacha salamaîalisema kiungo huyo.

Aidha Niyonzima amekiri kuwa tangu atue kucheza soka Tanzania hajawahi kukutana na mapokezi kama aliyopewa jambo ambalo mpaka sasa ameliweka akilini na kukosa mpinzani wake.

“Ilikuwa kitu cha tofauti sana, sijawahi kukiona kwenye mpira. Niliinamisha kichwa nilitokwa na machozi “Haitatokea tena kama ile, kwangu na kwa mchezaji mwingine yeyote hapa Tanzania,” alisema Niyonzima.

Hata hivyo ameeleza kuwa anafurahi kuona mpaka sasa bado yupo Tanzania na anacheza kwenye timu iliyompa heshima kubwa kwenye maisha yake ya soka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here