Home Habari NIYONZIMA AWAPA 5 SIMBA

NIYONZIMA AWAPA 5 SIMBA

685
0
SHARE

NA MWANDISHI WETU,

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima, amekuwa muungwana baada ya kutamka bayana kuwa kipigo cha mabao 2-1 walichokipata kutoka kwa Simba kilistahili kwani wenzao hao walikuwa wazuri zaidi.

Niyonzima ambaye Yanga wanamwita fundi kutokana na uwezo wake ndani ya uwanja, aliyasema hayo jana baada ya kumalizika kwa mpambano huo uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kiungo huyo alisema awali walikuwa wamewashika sana Simba hasa kipindi cha kwanza na kufanikiwa kupata bao 1-0 la kuongoza, lakini kipindi cha pili wapinzani wao hao wakaja juu na kuwazidi ujanja na kufanikiwa kuibuka na ushindi huo.

“Kwanza niwapongeze wenzetu kwa ushindi huo walioupata, lakini pia niseme tulijitahidi sana kipindi cha kwanza ila wenzetu wakaja juu kipindi cha pili na kufanikiwa kusawazisha na mwisho wa siku wakatufunga mabao 2-1,” alisema.

Akizungumzia mbio za ubingwa wakati huu ligi ikiwa inaelekea ukingoni, Niyonzima alisema mpaka sasa hakuna mwenye uhakika wa kulitwaa kombe hilo kutokana na ushindani mkubwa baina ya timu hizo mbili, lakini anaamini lolote linaweza kutokea kwa vile ligi bado inaendelea.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here