Home Habari Niyonzima: Tutakufa na Al Ahly Misri

Niyonzima: Tutakufa na Al Ahly Misri

514
0
SHARE

niyonzimaNA MWANDISHI WETU

BAADA ya kuwaangalia Al Ahly kwa dakika 90 akiwa jukwaani, kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima, ameibuka na kusema kuwa lazima awaadhibu Waarabu hao kwenye mchezo wa marudiano nchini Misri.

Niyonzima ambaye aliukosa mchezo wa kwanza wa Yanga dhidi ya Al Ahly kutokana na kuwa na kadi mbili za njano, ameliambia DIMBA kuwa ameshauona udhaifu wa Waarabu na hivyo anaomba Kocha Hans der Pluijm ampe nafasi tu.

“Nimewasoma kwa umakini na nimegundua wana mapungufu mengi hasa katika eneo lao la ulinzi. Si wazuri sana kwenye kukaba, hivyo naamini tutatengeneza nafasi nyingi sana kulekule kwao. Tutawapiga, labda kocha asinipange tu,” alisema Niyonzima.

Katika pambano la kwanza lililopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam na Yanga kulazimishwa sare ya bao 1-1, mashabiki wengi wa Yanga walitoka uwanjani wakilalamika kuwa kukosekana kwa Haruna ndio kumewanyima ushindi dhidi ya Waarabu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here