SHARE

NA JOSEPH SHALUWA    


LOVE Moment ni safu maalumu kwa wapendanao kukutana na kujifunza zaidi kuhusu mahusiano. Bila shaka umekuwa ukijifunza mengi kupitia safu hii na maisha yako yamebadilika kwa elimu unayoipata hapa.

Kama kawaida, leo tena ni siku nyingine nikiwa mwenye furaha sana ya kukutana nanyi wasomaji wangu wapenzi. Naomba kuchukua fursa hii kuwakaribisha kwa moyo mkunjufu katika safu yetu ambayo lengo lake hasa ni kuwekana sawa ili tuwe katika uhusiano bora wenye mafanikio badala ya matatizo.

Marafiki, wakati fulani unaweza kuwa kwenye uhusiano au ndoa na ukashangaa mwenzi wako hana muda na wewe. Kila unapotaka kumsogeza kwako, anageuka na kuendelea na mambo yako.

Inawezekana inakuumiza sana na huelewi sababu za mwenzako kufanya hivyo, lakini ukitulia na kujiuliza kwa makini utagundua kuwa kuna vitu ambavyo unavikosea, ndiyo sababu mwenzi wako anapoteza mshahawasha wa kuwa na wewe.

Kimsingi ni mada maalumu zaidi kwa wanandoa ambao kwa namna moja ama nyingine wanakosa furaha katika tendo la ndoa. Ninaposema hivyo namaanisha kuwa, wanakuwa na hamu ya kukutana na wenzi wao, lakini kwa bahati wenzi wao wanakuwa hawapo chumbani au hawatambui kuwa ubavu wake unahitaji kupumzika karibu yake.

Haya hutokea kwa wengi kwenye uhusiano, mwisho wake wengine hufikia hatua ya kuamini huenda mwenzi wake ana mpenzi mwingine, jambo ambalo halina ukweli, ila kuna makosa yamefanyika ama kwa kuelewa au kwa kutokujua.

Je, unajua namna ya kufanya ili kuweza kuvuta hisia za mwenzi wako? Je, unajua unatakiwa kuzingatia vitu gani ili mwenzi wako avutiwe na wewe na mshirikiane vyema faragha?

Kumbuka faragha ni kati ya vitu vya msingi sana kwenye ndoa. Ndoa ambayo haizingatii faragha au inafanyika holela ama isiyo na msisimko, ni rahisi kuingia kwenye migogoro.

Ili kuepukana na yote hayo, ni mambo gani basi muhimu kuzingatia ili kumsogeza karibu mwenzi wako na muwe na ndoa yenye furaha? Vipengele vifuatavyo vinafafanua kwa undani:

 

LUGHA YA MAPENZI

Mnapokuwa chumbani lazima lugha ya mapenzi itumike, mnapokuwa chumbani mnakuwa katika nchi nyingine yenye lugha nyingine na sheria nyingine, ila kuna wengine wanakuwa hawajapitisha sheria hizo katika uhusiano wao.

Wapo wanandoa wanaoishi na wenzi wao kwa muda mrefu lakini akihitaji penzi huogopa kumwambia mzee. Tatizo hapo mara nyingi huwa ni lugha ya mapenzi. Kutaka unataka, lakini ni kwa namna gani unafikisha hisia zako?

Kuogopa kusema au kuonyesha ishara ni ulimbukeni, ingawa inawezekana kulingana na mazingira ukashindwa kumwambia mzee unahitaji huduma yake.

Sasa basi, zipo lugha za mapenzi ambazo ukizitumia bila kumwambia mzee moja kwa moja atakuelewa na kukata kiu yako. Sasa tizama lugha hizo.

 

 

MAVAZI MWAFAKA

Mavazi maalumu ya faragha ni moja ya lugha ya mapenzi inayotakiwa kuzungumzwa chumbani. Wengi wamekuwa na mazoea ya kuvaa suruali, sketi fupi au kanga wakati wa kulala. Hii ni sawa, lakini siku ambayo unahitaji kukumbatiwa na mzee, lazima uonyeshe kuwa unahitaji!

Ukweli upo wazi kwamba mwanamume akimhitaji mwanamke ni rahisi tu, kwa sababu atakupapasa hapa na pale au wakati mwingine atakuambia moja kwa moja. Kwa upande wa wanawake ni vigumu, lakini kwa kutumia mavazi ni rahisi sana.

Mavazi yakitumika kwa ubunifu chumbani husaidia kuamsha hisia. Kwa mfano, nguo za ndani zenye msisimko, kanga nyepesi, night dress nk. Sasa basi, ni jinsi gani utapangilia mavazi hayo ili yalete hamasa? Hilo ni jambo jingine.

Wanawake wengi, hasa walioolewa wakishakaa ndani ya ndoa na kumzoea mwanamume huamua kujivalia mavazi yoyote ili mradi akiamini kuwa mume ameridhika naye, kumbe siyo kweli.

Mwanamke unahitaji ubunifu kila kukicha, kwani mwanamume anatoka na pia anakaa na wenzake, walio wengi husimuliana mambo yanayowapagawisha wawapo faragha.

Hapa nitazungumizia nguo za ndani, unajua unatakiwa kuvaa katika mpangilio gani? Hilo ni jambo jingine muhimu zaidi kulijua. Kulingana na nafasi iliyopo, wiki ijayo tutaendelea na mada hii. USIKOSE!

Je, ungependa kujifunza zaidi masomo haya kwa njia ya simu? Karibu ujiunge na group letu la WhatsApp. Tuma meseji kwenda namba 0718-400146, utaunganishwa.

Jiandae kupata kitabu changu kipya cha SIRI ZA MAISHA YA NDOA YENYE FURAHA kitakachokuwa mitaani hivi karibuni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here