Home Michezo kitaifa No Mata, No Party

No Mata, No Party

445
0
SHARE

MANCHESTER, England

JOSE Mourinho alirudi kwa mara ya kwanza Stamford Bridge na kupokelewa na kichapo cha aibu vijana wake wa Manchester United walichokipata kutoka kwa Chelsea.

Bila shaka kichapo cha bao 4-0 Man United walichokipata kutoka kwa Chelsea ni matokeo ya mbinu mbovu alizotumia Mreno Jose Mourinho. Aliyeigharimu United ni kocha wa United!

Mourinho aliingia Stamford Bridge kwa mbinu ile ile aliyoitumia kwenye pambano dhidi ya Liverpool, lililomalizika kwa matokeo ya 0-0. Kujilinda mwanzo mwisho!

Katikati ya uwanja, alipanga viungo watatu. Ander Herrera akiwa kiungo mkabaji, Marouane Fellaini akipangwa kama namba 8, huku Paul Pogba akicheza namba 10, nyuma ya straika mmoja wa mbele, Zlatan Ibrahimovic.

Ilichukua dakika 30 tu za mchezo Chelsea kubaini mapungufu ya mbinu za Mourinho na kupata matokeo. Kama si upangaji mbovu wa kikosi huenda Manchester United wangeweza kupata matokeo katika dimba la Stamford Bridge.

Kipindi cha pili, ‘Special One’ aligundua udhaifu wa kikosi chake na kufanya mabadiliko ya kumwingiza fundi wa Kihispania, Juan Mata na kumpumzisha Fellaini aliyeonekana kuchemka tangu dakika ya kwanza ya mchezo.

Yalikuwa mabadiliko sahihi lakini hayakufanywa kwa wakati sahihi, Juan Mata alitakiwa kuanza Stamford Bridge kutokana na takwimu nzuri alizokuwa nazo msimu huu.

Mara zote anapopata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza, Manchester United huwa hatari kwenye kutengeneza nafasi za kufunga.

Ni Juan Mata mwenye funguo ya furaha ya Jose Mourinho Old Trafford, ukweli uko hivyo. Mourinho anamuhitaji zaidi Mata kuliko Mata anavyoihitaji Man United muda huu. Kwanini?

United wamecheza mechi 9 msimu huu mpaka sasa na tano kati ya hizo, Juan Mata alipata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza.

Kwenye mechi 4 ambazo Mourinho amemweka benchi Mata, United wamepata pointi moja tu. Wamefungwa tatu na kutoka sare moja tu.

Na kwenye mechi 5 ambazo Juan Mata ameanza kwenye kikosi cha kwanza United wameshinda mechi 4 na kutoka sare moja, hawajafungwa!

Takwimu zinaonyesha kuwa kwenye mechi 5, Man United wamekusanya jumla ya pointi 13 kati ya 15. Kwanini Jose Mourinho hampi nafasi Mata kwenye kikosi cha kwanza?

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here