Home Michezo Kimataifa Novemba? Mwezi mbaya sana huu kwa Arsenal

Novemba? Mwezi mbaya sana huu kwa Arsenal

538
0
SHARE

LONDON, England

KAMA Arsenal wana nia ya kubeba taji msimu huu, jambo la kwanza wanalotakiwa kulifanya ni kuhakikisha wanafuta mkosi wao wa mwezi Novemba.

Tangu Arsene Wenger alipoichukua Arsenal mwaka 1996, washika mitutu hawa wa jiji la London wameshinda michezo 36 tu katika 78 waliyocheza mwezi huu.

Imekuwa kawaida kwa Arsenal kuanza vizuri msimu, kisha kuharibu kila inapofika mwezi Novemba, hivyo watalazimika kushinda michezo yao ya mwezi huu kujitengenezea mazingira mazuri ya kubeba taji msimu huu.

Mwezi huu Arsenal watapambana na mahasimu wao wa Jiji la London, Tottenham, kabla ya kuvaana na mashetani wekundu wa Old Trafford baada ya kumalizika kwa mapumziko ya wiki moja.

Baada ya hapo watakuwa kwenye uwanja wao wa Emirates, wakiikaribisha Bournemouth, kisha watapambana na PSG kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, mchezo wa mwisho wa Arsenal mwezi huu ni dhidi ya Southampton.

Ratiba ya Arsenal mwezi huu
Novemba 6: Arsenal v Tottenham – Premier League
Novemba 19: Man Utd v Arsenal – Premier League
Novemba 23: Arsenal v PSG – Ligi ya mabingwa
Novemba 27: Arsenal v Bournemouth – Premier League
Novemba 30: Arsenal v Southampton – Kombe la EFL

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here