SHARE

NA JESSCA NANGAWE

PATACHIMBIKA! Ndio kauli pekee kwa sasa kuhusu wasemaji wa vigogo wa soka nchini Haji Manara wa Simba na mwenzake Antonio Nugaz wa Yanga aliyetambulishwa rasmi juzi.

Ujio wa Nugaz ambaye ameajiriwa kama msemaji muhamasishaji ndani ya klabu hiyo umeanza kuzua gumzo, baada ya juzi kutoa kauli mbalimbali zinazomlenga mpinzani wake huyo na kuzua mjadala maeneo mbalimbali.

Akizungumza wakati wa kutambulishwa, Nugaz alisema anatambua uwezo wake na amekwenda pale kwa lengo kufanya kazi, si kushindana kama ambavyo wengi wanadhani.

Alisema uzoefu na elimu yake inatosha kuwaaminisha Wanayanga kuwa chuma kimetua na anawapa salamu wapinzani wao kwa kuongea kiuweledi na si kuropoka.

“Sisi hatushindani na mtu, tunakwenda kufanya kazi tuliyotumwa kiuweledi na si kuropoka, tunahitaji kuivusha Yanga kwenda nafasi nyingine kimaendeleo, tunajua imenyanyasika sana hapo kati lakini sasa tunasema unyonge kwisha,” alisema Nugaz.

Aidha Nugaz aliongeza wameanza na kauli mbiu ya #MsemajiKasema ikiwa na maana ya kufanya kazi kwa kutoshindana na mtu yoyote katika kazi zaidi ya kuchapa kazi.

Yanga imeajiri Ofisa Habari ambaye ni Hassan Bumbuli pamoja na Ofisa Uhamasishaji, Nugaz baada ya madai timu hiyo imekosa hamasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here