SHARE

NA VICTORIA GODFREY

KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Riadha Brunei Suleman Nyambui amekiri, kwamba viwango vya wanaridha nchini humo bado vipo chini na hawana uwezo wa kushiriki mashindano kimataifa.

Akizungumza na DIMBA Jumatano,kwa njia ya simu kutoka Brunei, Kocha Nyambui, alisema,sababu iliyochangia kutokuwa na viwango na maumbile yao si rafiki hususani mbio ndefu.

Alisema,tayari wameanza kuchukua hatua za kukabiliana na hilo ambapo wamegeukia katika kuwekeza mashuleni kusaka vipaji vitakavyoendelezwa kwa manufaa ya baadaye.

Nyambui, alisema, kwa kutumia walimu waliobobea kufundisha michezo mashuleni ili kuanza kupata wachezaji wa chini ambao watatengenezwa katika misingi iliyo bora kwakuwa na kambi za wiki tatu hadi nne mara baada ya shule kufungwa.

Kuna mkakati wa kuandaa mashindano ya kila ya baada ya miezi minne minne hii itasaidia kuwajenga na kuwapa uzoefu wa kushiriki mashindano yatakayowaongezea viwango vinavyostahili,îalisema Nyambui.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here