Home Burudani NYIE JOKATE ANAWAZA KUITWA MKE 2018

NYIE JOKATE ANAWAZA KUITWA MKE 2018

1074
0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE

MREMBO na mjasiriamali maarufu nchini, Jokate Mwegelo, ameanza kuota ndoto za kuitwa mke kwa mwaka huu licha ya kutoweka wazi uhusiano wake kwa sasa.

Mrembo huyo ameonyesha shauku ya kuwa mwaka huu anatamani kuitwa mke na kuanzisha familia yake maana muda unazidi kwenda.

Jokate alisema yupo tayari kukabiliana na majukumu hayo huku akizingatia masharti na vigezo katika kumpata mume aliye sahihi kwake.

“Natamani mwaka 2018 usinipite bila ya kuwa na mume, pia vigezo na masharti kuzingatiwa katika kumpata yule aliye sahihi kwangu,” aliandika Jokate.

Jokate amekuwa akihisiwa kuwa katika mahusiano na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Alikiba, kutokana na ukaribu walionao wawili hao licha ya kuwa wamekuwa wakipinga mbele ya vyombo vya habari kuwa hawapo kwenye mahusiano.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here