Home Michezo kitaifa OKWI AWATULIZA MASHABIKI SIMBA

OKWI AWATULIZA MASHABIKI SIMBA

2457
0
SHARE

NA CLARA ALPHONCE

STRAIKA wa Simba, Emmanuel Okwi, ametuliza presha ya mashabiki wa Wekundu hao baada ya kuwasili nchini akiwa fiti tayari kwa ajili ya mikikimikiki ya Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa.

Okwi hakuwa na timu kwa muda mrefu kutokana na kuwa majeruhi, na kwa mujibu wa rafiki yake wa karibu, alisema kuwa alitarajiwa kuwasili nchini jana usiku.

Licha ya kuwa na majeraha, lakini alikuwa na ruhusa ya kwenda kwao Uganda kwa ajili ya matatizo ya kifamilia ambayo yalipelekea kutokuwepo katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, ambapo Simba wametolewa katika hatua ya makundi na timu ya URA ya Uganda, baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0.

Licha ya michuano ya Mapinduzi, Okwi amekosa michezo miwili ya Ligi Kuu dhidi ya Mbao FC, ambapo walishinda 2-0 na ule wa Lipuli ambapo walitoka sare ya 1-1.

Kutokuwepo kwake huko kulizua taharuki nyingi kwa mashabiki wa klabu hiyo, ambapo wengi wao walikuwa wanaamini uwepo wake ungeongeza nguvu katika kikosi hicho na kufanya vizuri katika michuano hiyo.

Mshambuliaji huyo raia wa Uganda, anaongoza kwa ufungaji katika ligi akiwa amefunga mabao 8.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here