Home Habari Okwi hali ngumu Denmark

Okwi hali ngumu Denmark

1215
0
SHARE

NA EZEKIEL TENDWA

KAMA mshambuliaji wa zamani wa Simba na Yanga, Mganda Emmanuel Okwi, hatajumuishwa kwenye kikosi chake cha SonderjykE kitakachowavaa Horsens katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Denmark, atakuwa amekaa benchi mwezi mmoja na hivyo hali yake kuzidi kuwa tete.

Klabu yake ya zamani ya Simba ya Jijini Dar es Salaam, mara kadhaa imeeleza nia ya kutaka kumrejesha nyota wake huyo katika usajili wa dirisha dogo utakaofanyika hapo baadaye.

Katika klabu yake hiyo, Okwi hajacheza mchezo wowote wa ligi kati ya michezo mitatu waliyokwishacheza, ina maana akikosekana tena leo atamaliza mwezi mzima bila kutoa mchango wowote.

Katika mchezo wa kwanza wa mwezi huu uliochezwa Oktoba 2, dhidi ya Aab uliomalizika kwa SonderjyskE kuibuka na ushindi wa bao 1-0, Okwi hakuwepo hata nafasi ya kuwa mchezaji wa akiba, sawa na mchezo uliofuata walipoibuka na ushindi kama huo dhidi ya Vibro.

Mchezo wa mwishoni mwa wiki iliyopita walipocheza ugenini dhidi ya Lyngby na kukubali kichapo cha mabao 2-0, pia hakuwepo kabisa na leo anaweza kuukamilisha mwezi mzima kama hatavaa jezi kuwakabili Horsens.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here