SHARE

NA JESSCA NANGAWE

STRAIKA wa zamani wa Simba, Mganda Emmanuel Okwi, amekitaka kikosi cha Simba kusahau matokeo ya michuano ya kimataifa kwasababu ni kama wameteleza tu.

Okwi ambaye aliichezea Simba kwa mafanikio makubwa kabla ya kutimkia katika klabu ya Al Ittihad ya nchini Misri, bado ameendelea kuonyesha mapenzi yake kwa Wekundu hao wa Msimbazi.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Okwi alisema kukwama kwa kikosi hicho kusonga mbele katika michuano hiyo ni kuteleza tu kwasababu anatambua uwezo mzuri wa kila mchezaji aliyesajiliwa kwa sasa.

“Nadhani wameteleza tu, Simba ina kikosi imara na ambacho kingeweza kufika mbali zaidi ya mwaka jana ambapo tuliishia hatua ya robo fainali, nadhani kwasasa watulie wajipange na ligi ili waweze kutimiza mipango yao,” alisema Okwi.

Ndoto za Simba kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara nyingine zilizimwa Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa baada ya kukubali sare ya 1-1 katika mchezo wa marudiano dhidi ya UD Songo ya nchini Msumbuji.

Kwasasa kikosi hicho kilichopo chini ya kocha Patrick Aussems kimegeukia Ligi Kuu Tanzania Bara na kitatupa karata yake ya kwanza dhidi ya JKT Tanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here