Home Habari Omog aibukia mazoezini Yanga

Omog aibukia mazoezini Yanga

1183
0
SHARE

NA SAADA SALIM

SIKIA hii! Jina la Kocha Mkuu wa Simba, Mcameroon Joseph Omog, limetawala katika mazoezi ya timu ya Yanga baada ya mashabiki wa timu hiyo kujadili ufanisi wake wa kazi.

Majadiliano hayo yaliibuka jana asubuhi katika mazoezi ya Yanga yaliyofanyika Uwanja wa Boko Veterani, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Mashabiki hao waliokuwa wakishuhudia mazoezi ya timu yao walijikuta wakianza kujadili ujio wa Omog kwamba huenda akaibadili kabisa Simba msimu ujao.

Katika majadiliano hayo, mashabiki hao walisema Omog ni moja ya makocha wenye uwezo mkubwa na kwamba anaweza akaisaidia sana Simba msimu ujao lakini wakidai kuwa anaweza akakwamishwa na uongozi ambao mara kwa mara umekuwa ukiingilia kazi za benchi la ufundi.

“Huyo kocha (Omog) ni mzuri lakini kitakachomkwamisha ni tabia za viongozi wa watani zetu hawa kuingilia majukumu ya benchi la ufundi. Hata sisi kama Pluijm (Hans kocha wa Yanga) angekuwa anaingiliwa leo hii Yanga tusingekuwa bora namna hii,” alisema shabiki mmoja.

Mwingine akasema: “Hata mimi nakubali kwamba Omog ni mzuri kwani ndiye aliyewapa Azam FC ubingwa msimu wa 2013/14, lakini pale Simba hataweza kwani lazima ataingiliwa majukumu yake.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here