Home Habari onas Mkude MIAKA SITA SIMBA MECHI MOJA YA KIMATAIFA

onas Mkude MIAKA SITA SIMBA MECHI MOJA YA KIMATAIFA

1514
0
SHARE

NA SAADA SALIM

UTAWAAMBIA nini mashabiki wa klabu ya Simba juu ya kiungo mzawa Jonas Mkude? Nahodha huyo wa zamani wa Wekundu hao Msimbazi ni mmoja wa wachezaji vipenzi kwa timu hiyo.

Hakuna shabiki wa Simba unaweza kumdanganya kitu kuhusu uwezo wa Mkude dimbani ambaye amedumu na timu hiyo tangu mwaka 2012 alipopandishwa kutoka kikosi cha pili kuja kupokezana namba na Mwinyi Kazimoto.

Achana na kipindi kigumu cha sasa anachopitia akisugulishwa benchi na Kocha Mcameroon, Joseph Omog, ukweli ni kwamba Mkude ni mmoja wa viungo bora wenye uwezo mkubwa wa soka nchini.

Kitu pekee ambacho pengine unaweza ukawa hukijui kuhusu Mkude ni kwamba jamaa kwa misimu yote sita aliyoichezea Simba, ameichezea timu hiyo mechi moja tu ya mashindano ya kimataifa.

Mechi anayoikumbuka ni ile ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi na Es de Setiff mwaka 2012. Ikumbukwe mwaka wa mwisho Simba kushiriki michuano ya kimataifa ilikuwa mwaka 2013 iliposhiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kutolewa CR Libolo ya Angola baada ya kufungwa kwa mabao 4-0.

BREAKING News imemnasa Mkude na kuteta naye mambo kadhaa ambapo anaeleza mechi yake ya kimataifa kucheza ilikuwa 2012.

“Tulipocheza Dar es Salaam Saint Setiff, nakumbuka niliingia uwanjani kuchukua nafasi ya mtu nikitokea benchi, ilikuwa mechi yangu ya kwanza ya kimataifa kucheza.

“Ukiangalia nilikuwa bado ni mdogo halafu ni mchezaji pekee nisiyekuwa na uzoefu na mechi za kimataifa, kabla ya kuingia kocha aliniinua na kuniambia nisome mchezo vizuri kwani natakiwa kwenda kuziba nafasi ya mchezaji aliyetolewa,” anasema.

USHIRIKI WA SIMBA KIMATAIFA:

Mkude anasema kwa sasa hakuna ubishi kuhusu upana wa kikosi chao kwani wana wachezaji wazuri na wenye uzoefu mkubwa wa kukabiliana na michuano ya kimataifa.

“Nadhani kwa sasa Simba imepanuka zaidi kwani ukiangalia wachezaji wake wazuri ni imani yangu, tunapokutana na timu ambazo zinatusumbua tutakabiliana nazo kutokana na uzoefu tulionao,” anasema Mkude

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here