SHARE

Lulu Ringo, Dar es salaam.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba Sc wameendelea kujifua katika Uwanja wake wa Boko Veterani kujiandaa na mechi mbili za kirafiki moja ya Dar es Salaam na nyingine kutoka nje ya Tanzania.

Akizunguza na waandishi wa Habari, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Patrick Aussems amesema licha ya mapumziko hayo mafupi kwa ajili ya timu ya taifa kikosi chake kitaendelea na mazoezi pamoja na kucheza mechi za kirafiki ili kuisaidia kujiweka sawa na Ligi Kuu itakapoendelea.

“Kwangu hakuna kupumzika kama kuna timu imepumzisha wachezaji wake basi ina matatizo, wachezaji wangu wataendelea na mazoezi kama kawaida na tunatarajia kuwa na mechi ya kirafiki na timu ya Ligi daraja la pili siku ya Ijumaa na siku zijazo nitawajuza tunaweza kuwa na mechi nyingine kutoka timu nje ya Tanzania,” amesema Aussems.

Kikosi cha Simba kilichofanya mazoezi siku ya leo ni Magolikipa Deogratius Munishi na Said Nduda, Mzamiru Yasini, Said Hamis, Haruna Niyonzima, Rashid Juma, Mohamed Ibrahimu, Mohamed Rashid.

Wengine ni Mohamed Hussein, James Kotei, Hassan Dilunga, Marcel Kaheza, Yusuph Mlipili, Poul Bukaba na Pascal Wawa.

Kocha huyo pia amesema wachezaji wake 14 wapo nje ya kikosi chake kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kujiuguza kwa wale majeruhi na wengine wamejiunga na timu zao za Taifa

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here