SHARE
Lille's Ivorian forward Nicolas Pepe celebrates after scoring a goal during the French L1 football match between Lille (LOSC) and Olympique Lyonnais (OL) on December 1, 2018 at the Pierre Mauroy Stadium in Villenueve d'Ascq. (Photo by FRANCOIS LO PRESTI / AFP) (Photo credit should read FRANCOIS LO PRESTI/AFP/Getty Images)

LONDON, England

MCHEZAJI ghali ndani ya kikosi cha Arsenal, Nicolas Pepe amewashukia wachezaji wenzake huku akiwataka wajitume zaidi kama wanataka kufanikiwa ikiwezekana kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Pepe alijiunga na Arsenal msimu huu kwa dau la pauni milioni 72 akitokea Lille, winga huyo ambaye ameanza kuonesha kiwango kizuri hivi karibuni amedai wana uwezo wa kufanya vizuri kama wataweka uzembe pembeni.

“Inaweza kuwa ngumu lakini hakuna ambacho kinashindikana, tukionesha kiwango kizuri na kupata matokeo tutafanikiwa kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

“Nafasi bado ipo wazi, tukiacha uzembe tutafanikiwa zaidi, mafanikio yanapatikana kwa kujituma,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here