SHARE
PHIRI

NA JESSCA NANGAWE


KIKOSI cha Mbeya City kimemaliza mechi zake za kirafiki mwishoni mwa juma na sasa kimeelekeza nguvu zake katika mechi za ligi kuu, ambapo kocha mkuu wa timu hiyo, Kinnah Phiri, ameanika mikakati yake.

Kikosi hicho chenye maskani yake katika Jiji la Mbeya, kitakuwa na kibarua kigumu watakapowakabili Azam FC katika mchezo unaokuja, ambapo kocha huyo amesema lazima washinde kwani malengo yake ni kuifanya timu hiyo kumaliza moja ya nafasi tano za juu.

Phirri alisema wametumia vyema mechi za kirafiki kukipima kikosi hicho na wapo tayari kukutana na vigogo wa ligi kuu ili kusaka nafasi tano za juu na hilo linawezekana kutokana na uwezo wa wachezaji wake.

“Tunamshukuru Mungu kwamba tumecheza michezo kadhaa ya kirafiki wakati ligi iliposimama na yale mapungufu yaliyokuwepo tumeyafanyia kazi, kilichobakia ni kupambana katika ligi kwani ninachokihitaji ni kuona tukimaliza moja ya nafasi tano za juu msimu huu,” alisema.

Katika msimamo wa ligi hiyo, Mbeya City wanashika nafasi ya sita wakiwa na pointi 24 kwenye michezo 18 waliyoicheza, wakifanikiwa kushinda michezo sita, sare sita na kupoteza michezo sita.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here