Home Makala PIERLUIGI COLLINA HANA MFANOWE

PIERLUIGI COLLINA HANA MFANOWE

6615
0
SHARE

NA NIHZRATH NTANI JNR


JIONI moja ya mwaka 1977 ndani ya Mji wa Bologna nchini Italia, vijana wadogo wenye umri kati ya miaka 15-18, walikuwa na mechi kati yao. Mechi yao iliwakutanisha watoto wa kutoka sehemu ya Tuscany na wale kutoka eneo la Forte du Marmi.

Ni mechi iliyojaa upinzani mkubwa kwa vijana hao jioni hiyo. Hata hivyo, mechi hiyo haikumalizika katika muda sahihi, baada ya kujaa maamuzi mengi  yenye utata. Mwamuzi alionekana kuwabeba mno vijana kutoka katika eneo la Forte du Marmi.

Ndani ya timu ya wavulana kutoka eneo la Tuscany, mvulana mwenye umri wa miaka 17 wakati huo, alionekana kuchukizwa mno na maamuzi mabaya kutoka kwa mwamuzi dhidi ya timu yake.

Kijana huyu alicheza nafasi ya kiungo ndani ya timu hiyo. Hasira za kijana huyu zilimfanya aanze kuuchukia mchezo wa soka. Aliamini kuwa mchezo wa soka hauna haki.

Chuki dhidi ya mwamuzi yule zikamfanya aukache mchezo wa soka na badala yake akaelekeza nguvu kucheza mchezo wa basketball.

Marafiki zake walijaribu kumshawishi kurejea katika soka. Ushawishi wao haukuleta maana kubwa ndani ya akili ya mvulana yule. Alisimamia alichokiamini.

Miezi michache ndani ya mwaka 1977, marafiki zake walewale wakajaribu tena kumshawishi  kwa mara nyingine angalau ajifunze kuwa mwamuzi ili aweze kutenda haki kama anavyoazimia.

Ombi hili lilipokelewa kwa tabasamu lenye kumaanisha ndani ya akili ya kijana yule. Ndipo alipoamua kuanza kuhudhuria kozi ndogo ndogo za uamuzi wa soka ndani ya Mji wa Bologna.

Miaka 27 baadaye tangu ombi la kuanza mafunzo ya uamuzi wa soka kulikubali, kijana yule alikuwa anastaafu kazi ya uamuzi katika soka. Ajabu iliyoje!

Pamoja na kustaafu kwake kwa mujibu wa sheria, lakini uamuzi huo ulileta simanzi na huzuni kubwa kwa wadau na mashabiki wengi wa soka duniani.

Akiwa na miaka 45 hadi kufikia mwaka 2005 alipostaafu huku akiwa na miaka 58 hivi leo, kijana yule ndiye huyu anayeitwa Pierluigi Collina. Huhitaji kufungua vitabu vingi vya historia kujua mtu huyu alikuwa nani?

KWANINI NIMEAMUA KUMZUNGUMZIA PIERLUIGI COLLINA?

Unahitaji mistari miwili au mitatu kujaza makosa yake dimbani. Lakini unaweza kuhitaji kurasa zenye kujaza kitabu kizima kuweza kuuandika umakini  na ukamilifu wake dimbani.

Ni kwamba alikuwa na makosa machache zaidi wakati alipokuwa akichezesha soka. Bila shaka Pierluig Collina aliishi katika mtazamo na ndoto aliyoiota angali kijana mdogo zaidi. Ndoto ya kuona haki ikitendeka uwanjani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here