Home Habari PLUIJM AANZA NA KUTINYU AZAM

PLUIJM AANZA NA KUTINYU AZAM

1618
0
SHARE

NA MAREGES NYAMAKA


BAADA ya sare ya 0-0 waliyokumbana nayo Azam dhidi ya URA ya Uganda, ikiwa ni mchezo wa kirafiki kama maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania, Kocha wao, Hans van der Pluijm, ameonekana kuifungia kazi safu ya kiungo.

AZAM FC juzi walicheza mechi yao ya kwanza nchini Uganda dhidi ya URA, ikiwa ni mwendelezo wa kambi waliyoiweka nchini humo kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu.

Katika mechi hiyo iliyomalizika kwa matokeo ya suluhu 0-0, kocha wa kikosi hicho, Hans van der Pluijm, hakuridhishwa na matokeo hayo, hivyo ameamua kufanya marekebisho, hasa sehemu ya kiungo, yenye wachezaji kama Tafadza Kutinyu, Mudhathir Yahya, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na Frank Domayo.

Pluijm aliliambia DIMBA ulikuwa ni mchezo wa ushindani, akidai timu ilicheza vizuri kiasi fulani, lakini bado kuna mapungufu aliyoyaona, hasa safu ya kiungo na hivyo ameamua kulifanyia kazi eneo hilo.

“Tulishindwa kutengeneza nafasi na hapo ukitazama ni safu ya kiungo ndiyo iliyokuwa na jukumu la kwanza la kupenyeza mipira, siwezi kuwalaumu sana kwa kuwa uwanja nao haukuwa rafiki, lakini bado haiwezi kuwa sababu kubwa, kwani ni sawa na viwanja vyetu vingi tunavyochezea ligi Tanzania,” alisema.

Ziara ya matajiri hao wa Bongo chini humo imebaki wiki moja,  ambapo watacheza mechi nyingine tatu za kirafiki kabla ya kurejea nyumbani kwa maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza kwa ligi Agosti 22.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here