SHARE

NA MWANDISHI WETU


WAKATI Azam FC, wakijitupa katika Uwanja wao wa Azam Complex kesho kuwakabili Coastal Union ya jijini Tanga, kocha Mkuu wa Wanalambalamba hao Hans Van de Pluijm, ameibuka na kudai kuwa, kwa sasa hana tena masihara katika mechi yoyote, hivyo timu hiyo ijipange.

Akizungumza na Dimba, Pluijm, ambaye ni kocha mzoefu katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara, alisema amewapanga vijana wake vizuri kuhakikisha wanashinda mchezo huo ili kuzidi kujikusanyia pointi.

“Kwetu sisi tumejipanga vizuri kuhakikisha tunapata matokeo mazuri michezo yetu yote, sio huo mmoja tu, bali yote, ndiyo maana tumekuwa tukifanya maandalizi mazuri,” alisema.

Mpaka sasa Azam FC, wameshacheza michezo saba, wakishinda minne na kutoka sare mitatu, wakijikusanyia jumla ya pointi 15, wakiwa hawajapoteza mchezo wowote na kujikita nafasi ya pili katika msimamo wa ligi.

Katika mchezo huo wa kesho, Pluijm ataitegemea zaidi safu yake ya ushambuliaji, hasa baada ya Straika Mzimbabwe, Donald Ngoma, kurejea kwa kishindo akionyesha soka safi katika michezo miwili aliyocheza msimu huu.

Kwa upande wao Coastal Union, wamecheza michezo minane, wakishinda mitatu na kufungwa mchezo mmoja, pia kutoka sare michezo minne ambapo Kocha wao Mkuu, Juma Mgunda, naye ametamba kwamba wanataka kurudi Tanga na pointi tatu kutoka kwa matajiri hao wa Chamazi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here