Home Burudani PLUIJM AFUMUA KIKOSI AZAM FC

PLUIJM AFUMUA KIKOSI AZAM FC

8617
0
SHARE

NA SAADA SALIM


 

KOCHA Mkuu wa Singida United, Hans van der Pluijm, anatarajiwa kujiunga na Azam FC baada ya msimu huu kumalizika na taarifa zisizo na shaka zinadai Mholanzi huyo ameanza kupeleka mapendekezo ya kikosi chake kipya cha msimu ujao.

Moja ya mapendekezo hayo ni kwamba wale wachezaji wote wasio na viwango vya kuridhisha waondoke mapema na tayari Wanalambalamba hao wameanza na straika wao, Mghana Bernard Arthur,    ambaye amefungashiwa kila kilichochake.

Azam wamesitisha mkataba na straika huyo baada ya kushindwa kuonyesha ubora katika kipindi cha nusu msimu, alichoitumikia timu hiyo huku taarifa nyingine zikidai kuwa bado kuna panga kali litapita.

Taarifa hizo zinadai kuwa kitendo cha uongozi huo kusikitisha mkataba wa Mghana huyo, ni kutokana na mapendekezo ya Pluijm ambaye anatarajiwa kurithi mikoba ya Mromania, Cioaba Aristica anayemaliza mkataba wake Julai mwaka huu.

Akizungumzia namna walivyomtema mchezaji huyo kutoka Ghana, Makamu Mwenyekiti wa Azam, Abdulkarim Amin `Popat`, alisema ilikuwa ni makubaliano ya pande zote mbili hivyo taratibu zilifuatwa.

Taarifa za uhakika zilizolifikia DIMBA Jumatano kutoka ndani ya timu hiyo zinadai kwamba, tayari mazungumzo kati ya Pluijm na uongozi wa Azam yamefikia pazuri na kilichobakia ni yeye kumalizana na Singida United msimu huu ili kuanza maisha mapya ndani ya Wanalambalamba hao.

“Moja ya mapendekezo yake ni kuhakikisha wanafumua kikosi kwa kuwaondoa wachezaji ambao hawana nafasi na kuleta wenye uwezo mkubwa, yeye pia anayo majina yake atakayokuja nayo ya wachezaji tutakaowasajili,” alisema kigogo mmoja ndani ya Azam FC.

Kama Pluijm atamalizana na Azam FC, huenda akaidhoofisha Singida United kwa kuondoka na baadhi ya wachezaji muhimu akiwamo Deus Kaseke ambaye anakubali sana aina ya uchezaji wake pamoja na Mudathir Yahya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here