Home Habari PLUIJM AIPASUA YANGA

PLUIJM AIPASUA YANGA

305
0
SHARE

NA MWANDISHI WETU,

SAA chache baada ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, Yanga kumtupia virago Mkurugenzi wao wa ufundi, Hans van der Pluijm, kumeibuka mpasuko mkubwa wa kimtazamo baina ya viongozi, wanachama na mashabiki wa timu hiyo.

Pluijm kabla ya kupewa nafasi ya ukurugenzi, alikuwa kocha mkuu wa timu hiyo na kuipa mafanikio kwa kutwaa taji la Ligi Kuu mara mbili mfululizo na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) huku pia akiifunga Simba mara mbili misimu hiyo ikiwa ni mbali ya Ngao ya Jamii.

Baadhi ya viongozi na mashabiki waliozungumza na DIMBA kwa nyakati tofauti, walisema kwa hali ilivyo Pluijm alitakiwa kubaki kwa kuwa pamoja na mambo mengine anaijua vyema Yanga na pia ni mwanachama wa Yanga hivyo angeweza kuivumilia timu hiyo katika kipindi hiki cha mpito.

“Ninaamini kwamba Pluijm alitakiwa kubaki, Yanga inawania kutetea ubingwa na kufanya vyema michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na yeye ni mtu anayeijua vyema klabu ikiwa ni pamoja na kujua hali ya uchezaji wa mechi za mikoani.

“Kufukuzwa kwake kipindi hiki tukiwa kwenye vita nzito nahisi tumejiweka pagumu katika mbio zetu, haikuwa sahihi, ni bora angeondoka Lwandamina (George) kama lengo ilikuwa ni kupunguza gharama,” alisema mwanachama Athumani Saidi wa Tandale.

Wakati wengine wakiwa kwenye mtazamo huo, wengine wanaunga mkono suala la klabu hiyo kuachana na Mholanzi huyo kwa madai mbalimbali ikiwemo tuhuma za kuwagawa wachezaji ambazo zilianza kuibuka baada ya ujio wa Lwandamina hali iliyosababisha uongozi wa Yanga kumzuia Pluijm kuzungumza na wachezaji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here