Home Makala PLUIJM NI KOCHA SAHIHI KWA AZAM?

PLUIJM NI KOCHA SAHIHI KWA AZAM?

706
0
SHARE

WIKI iliyopita uongozi wa Azam uliamua kuwafungashia virago makocha wake kutoka nchini Hispania, kutokana na kutoridhishwa na utendaji kazi wa makocha hao na mwenendo mbaya wa timu hiyo kwenye michuano ya Ligi Kuu Bara inayoendelea.

Jopo hilo la makocha lilikuwa linaundwa na Kocha Mkuu, Zeben Hernandez, Msaidizi wake, Yeray Romero, Kocha wa Makipa Jose Garcia, Kocha wa Viungo, Pablo Borges na Mtaalamu wa tiba za viungo, Sergio Perez, wote kutoka Hispania.

Hernandez anaondoka Azam FC akiwa ameiongoza timu hiyo kwenye mechi 18 ambazo ni za mashindano, 17 za ligi na moja ya Ngao ya Jamii, amefanikiwa kushinda mechi nane, sare sita na kufungwa mara nne.

Makocha hao waliajiriwa Mei mwaka huu wakichukua nafasi ya Mwingereza, Stewart Hall, aliyeamua kuachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu uliopita.

Hata hivyo, Azam inahusishwa na kumchukua kocha wa zamani wa Yanga, Hans van der Pluijm, ambaye kwa sasa amepewa jukumu la Ukurugenzi wa benchi la ufundi kwenye timu hiyo.

Habari za chini ya kapeti zinasema tayari mazungumzo baina ya pande mbili hizo yaani uongozi wa Azam na Pluijm mwenyewe yanaendelea ambapo kocha huyo amekubali kuinoa timu hiyo.

Japo Azam wenyewe bado hawajaweka wazi jambo hilo, lakini suala hilo lipo kwani timu hiyo ilianza kumuwinda Pluijm kwa muda mrefu.

Ukiwa kama mdau wa soka nchini unadhani Pluijm ni kocha sahihi kwa Azam? Anaweza kuisaidia timu hiyo kwenye Ligi Kuu na hata michuano ya kimataifa inayokabiliwa nayo?

Tuma maoni yako ukianzia na jina lako kamili na mahali unapoishi.

RAIS WA KIJIWE, 07669734494

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here