SHARE

LISBON, URENO

KLABU ya FC Porto imemjumuisha katika kikosi chake cha msimu ujao kipa Iker Casillas ambaye anasumbuliwa na shambulio la moyo.

Nyota huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania na klabu ya Real Madrid mwenye miaka 38 ni miongoni mwa majina yaliyowekwa hadharani katika blogu na website ya klabu hiyo.

Casillas, nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania aliyeisaidia timu hiyo kutwaa taji la Kombe la Dunia mwaka  2010 aliyejiunga na  Porto mwaka  2015, anasumbuliwa na shambulio la moyo ambapo kwa mara ya kwanza lilimtokea Mei 1 mwaka huu  na kukaa hospitali siku tano.

Rais wa Porto, Jorge Nuno Pinto da Costa, alidhani huenda huo ungekuwa mwisho wa mkongwe huyo jambo lililofanya waanze kusaka mbadala wake.

Licha ya kumbakisha mkongwe huyo tayari Porto wamemsajili kipa wa timu ya taifa ya Argentina, Agustin Marchesin kutoka Club America ambaye tayari ameisaidia klabu hiyo kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Krasnodar katika mchezo wa kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here